RAIS KIKWETE AMTEUA BALOZI MANONGI KWENDA UN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Tuvako Manongi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 25, 2012 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza jana, Julai 24, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Balozi Manongi ambaye ni ofisa wa miaka mingi wa masuala ya nchi za nje, alikuwa Mshauri Mwandamizi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York.
Balozi Manongi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 30, mwaka jana, 2011.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Julai, 2012
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !