CHANZO:MWANANCHI.
Posted
Jumapili,Mei19 2013 saa 21:8 PM
Dar
es Salaam.
Askofu
wa Kanisa Katoliki,Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo amewataka waumini wa kanisa hilo kutoogopa kifo badala yake waendelee
kwenda makanisani licha ya kuwapo kwa vitisho vya kushambuliwa.
Pengo
alisema hayo jana katika Kanisa la Mtakatifu Joseph alipokuwa akitoa sakramenti
ya kipaimara na aliwataka wasiwe na hofu lakini waendelee kumwamini Yesu Kristo
kama Mwana wa Mungu.
“Tuendelee
kwenda makanisani,kamwe tusiogope kuuawa,tuwe na imani kwamba Yesu Kristo ndiye
mlinzi wetu na ndiye atuongozaye,”alisema Pengo.
Kardinali
Pengo alisema hata kama vyombo vya dola vitakuwa vimeshindwa kuwalinda,waumini
kamwe wasiache kwenda makanisani kwa ajili ya kuabudu.
Pengo
aliwataka waumini hao kutolipiza kisasi kutokana na mauaji yaliyotokea hivi
karibuni mkoani Arusha kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya
Yesu Kristo.
“Wakristo
kulipa kisasi ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kikristo na sheria za
nchi,” alionya Pengo.
Kauli
hiyo imekuja baada ya watu watatu kuuawa kwa bomu na wengine zaidi ya 60
kujeruhiwa hivi karibuni katika Kanisa Katoliki,Parokia ya Joseph
Mfanyakazi,Olasiti nje kidogo ya jiji la Arusha.
Mauaji
hayo yalitanguliwa na kuuawa kwa Padri Evarist Mushi aliyeuawa Februari 17
wakati akielekea katika Kanisa la Mtakatifu Theresia,Zanzibar kuendesha misa.
Pia
Desemba 25 mwaka jana,Padri Ambrose Mkenda alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi
watu wasiojulikana wakati akisubiri kufunguliwa geti nyumbani kwake Zanzibar.
Pengo
aliwataka waumini wote kuendelea kusali kwa imani yao na kwamba matatizo
yanayojitokeza yasiwakatishe tamaa.
Alisema
hata katika mafundisho, kuna mambo mengi ambayo yalifanywa na baadhi ya watu
ili kumkatisha tamaa Yesu Kristo asitimize malengo yake lakini baadaye alishinda.
“Vivyo
hivyo waumini yanayojitokeza hivi sasa yasitukatishe tamaa tuendelee na
utaratibu wetu wa siku zote na tutashinda,”alisema Pengo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !