Wamtaka JK kutoa msimamo wa kisheria kwa Uislamu,
Ukristo.
Na Nora Damian,
Mwananchi )
Posted Mei4 2013 saa 24:45 AM
Posted Mei4 2013 saa 24:45 AM
0
inShareJukwaa la Wakristo Tanzania limemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wake kisheria ambao utaleta upatanisho kati ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo.
inShareJukwaa la Wakristo Tanzania limemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wake kisheria ambao utaleta upatanisho kati ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo.
Jukwaa
hilo limesema kauli iliyotolewa na rais juzi wakati wa sherehe za Mei Mosi,
Mbeya ya kutaka Watanzania waishi kama zamani ina utata kwa sababu imetafsiriwa
tofauti na baadhi ya Watanzania.
Hivi
karibuni Rais Kikwete wakati akizungumza kwenye sherehe za Mei Mosi alisema
Serikali bado inaendelea kuzungumza na viongozi wa dini wa pande zote na
kuwaunganisha ili kuona maelewano yanarejea kama ilivyokuwa zamani na kuwataka
Watanzania waendelee kuishi bila kubaguana au kuchukiana kwa dini zao.
Akizungumza
jana, Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye pia ni
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kikatoli Tanzania (TEC), alisema licha ya maneno
hayo kuwa mazuri lakini bado kuna utata kwa sababu baadhi ya raia wameingiwa na
wasiwasi.
Alisema
maeneo mengine wakristo hawali nyama kwa sababu hawataki kulazimishwa kula
nyama zilizochinjwa kwa ibada za kiislamu na kwamba suala hilo siyo dogo kama
wengine wanavyofikiri kwa sababu limegharimu maisha ya watu.
Alisema
licha ya kuwapo kwa kauli za uchochezi wa kuwaua viongozi wa dini ya
kikristo,kuchoma makanisa na mauaji ya viongozi wa kikristo bado hazijafutwa
wala waliozitoa hawajakamatwa na kwamba hawajui kinachoendelea.
Mwenyekiti
huyo alisema madai ya msingi ya waislamu yaliyosababisha waanzishe vurugu na
mauaji hayajajibiwa na Serikali huku maswali yaliyoulizwa na wakristo kutokana
na madai hayo na vurugu hizo nayo yakiwa hajayajibiwa.
Alisema
licha ya kukutana na Rais Kikwete Aprili 23, mwaka huu ambaye alihimiza
viongozi wa wakristo na waislamu wakutane ili kuondoa tofauti zao zisizo za
kiimani lakini bado wanasubiri maelekezo toka serikalini kwani ajenda ya
uvunjifu wa amani viongozi wa dini hawawezi kuizungumzia kwa sasa bila majibu
ya Serikali kwa madai yaliyozua uvunjifu huo wa amani.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !